
Sign up to save your library
With an OverDrive account, you can save your favorite libraries for at-a-glance information about availability. Find out more about OverDrive accounts.
Find this title in Libby, the library reading app by OverDrive.

Search for a digital library with this title
Title found at these libraries:
Library Name | Distance |
---|---|
Loading... |
RONIN 1 - UPANGA
Mvulana anaamka katikati ya msitu. Hajitambui au kutambua jinsi alivyofika pale. Kwa usaidizi wa watu tofauti na wanyama, na pia mkuki ulio na uwezo wa kipekee, Ronin huyu anapitia matukio mengi. Wakati ambapo kijiji kinahitaji ulinzi wake, lazima ajifunze kupigana kwa heshima ya wakulima anaowaokoa, na kwa ajili yake mwenyewe. RONIN 2 - UTA
Ronin anakutana na rafiki wa zamani na anaanza kujifunza kwa kutumia sensei wake, ambapo anajifunza kuwa hakuna lisilowezekana. Matukio yake yanakuwa mengi anapokuwa akiwatetea wanyonge na akiutumia uwezo wake vyema. Ronin anajifunza mengi kuhusu yeye mwenyewe, na inawezekana, pia kuhusu anakotoka. RONIN 3 - MKUKI
Ronin anakumbana na changamoto kali na kujifunza kuwa wakati mwingine, hata katika maadui, kuna mengi zaidi ya tunavyofikiri. Anapojifunza kuhusu maisha yake ya zamani, baba yake na mkuki, maswali mengi zaidi yanaibuka. Katika tukio la hivi karibuni, Ronin alikaribia kujua yeye ni nani na jinsi gani anaweza kuwasaidia wale wote anaowajali sana. RONIN 4 - KUCHA
Ronin anaendelea na safari yake ya kuelekea Meifumado. Njiani, anashambuliwa na maadui ambao ni waovu zaidi kuliko chochote ambacho aliwahi kukutana nacho. Akiungana na marafiki zaidi, analazimika kufanya uamuzi mgumu na kuvishinda vikwazo vyake vigumu zaidi. RONIN 5 - KUONYESHA
Katika sehemu ya mwisho ya mfululizo wa Ronin, Ronin anasafiri kwenda Meifumado kukutana na hatima yake na kuyaokoa maisha ya Azami. Ni kwa kupigana na Kivuli cha Mfalme na jeshi lake la mapepo wabaya ambapo Ronin anajifunza kuhusu mambo yake ya kale, familia yake na jinsi anavyoweza kutenda kulingana na jinsi alivyo na jinsi anavyoamini. Katika hali ngumu zaidi, lazima Ronin akumbuke jinsi shujaa wa kweli anavyopaswa kuwa.