Sign up to save your library
With an OverDrive account, you can save your favorite libraries for at-a-glance information about availability. Find out more about OverDrive accounts.
Find this title in Libby, the library reading app by OverDrive.

Search for a digital library with this title
Title found at these libraries:
Library Name | Distance |
---|---|
Loading... |
Baada ya kufanya kazi za upelelezi wa muda mrefu, akihusika na mambo yanayohusiana ndani ya nchi ya Tanzania. Tatizo kubwa lilitokea, ni baada ya kufika taarifa ya usaliti wa jasusi mmoja wa EASA aliyetorokea jimbo la Juba kusini mwa Somalia.
Taarifa inasemekana alimjeruhi mwenzake vibaya, ambaye alitibiwa na kupona na alibaki nchini Kenya akiendelea na kazi zingine. Wakati huyo msaliti akiendelea kujichimbia nchini Somalia.
Inaandaliwa operesheni, aliyotakiwa mpelelezi mmojawapo atumwe kwenda huko. Huyo aihitajika kufika mjini Lamu aonane na jasusi aliyejeruhiwa, ambaye angekuja kumsafirisha kwa kutumia watu wake kwenda Juba. Huko wangekuja wapelelezi wengine ambao wangeigiza kama wanamgambo, hao wangemteka na kumfikisha kwenye kundi mojawapo la wanamgambo huko ndiyo angefanya kazi yake.
Shirika lilimteua Norbert Kaila kushikilia jukumu hilo, ambaye aliondoka nchini Tanzania kwa mujibu wa itifaki ilivyo. Ila mambo yanakuja kugeuka baada ya kufika nchini Somalia. Huko anatekwa kibaya zaidi wanaofanya kazi hiyo ni majambazi kamili wa kundi mojawapo, na si wale wenzake ambao walipangwa kufika huko.
Watekaji waliwahi mapema kabla ya majasusi wengine, walitimiza jukumu hilo, mwisho wake ikaja kuwa tatizo kubwa kwa EASA. Norbert Kaila aliwekwa nguvuni, inampasa kujiokoa na kuendelea na misheni yake.