Sign up to save your library
With an OverDrive account, you can save your favorite libraries for at-a-glance information about availability. Find out more about OverDrive accounts.
Find this title in Libby, the library reading app by OverDrive.

Search for a digital library with this title
Title found at these libraries:
Library Name | Distance |
---|---|
Loading... |
Ajali mbili zinatokea kwenye majira tofauti, zote zikiondoka na maisha ya watumishi wa umma kutoka taasisi ambazo zina ukaribu kwenye ufanyaji kazi. Baada ya tukio hilo kunafuatia kutangazwa ufisadi uliyowahusu watumishi wao. Ikielezwa walipanga uhaini mkubwa, na walichota kiasi kikubwa cha pesa za serikali.
Mmoja ilielezwa alifikwa na ajali akiwa mafichoni mbugani alipofika kama mtalii. Mwingine ikitajwa alikuwa akikimbia kuelekea kujificha, ndiyo hapo alifikwa na mauti akiwa njiani. Ikawa habari iliyoshika hisia za wengi, kiasi cha kuibua wanaharakati na watu wa mitandaoni baada ya kuachiwa makala toka kwa mwandishi wa habari za kiuchunguzi.
Suala hilo lilimvutia Norbert Kaila baada ya kuona lilikuwa likihusu ubadhirifu, alitaka kufanya utafiti na kuweka kila kitu wazi. Alipoingia kwenye kazi hiyo, ndiyo hapo alikuja kukutana na mengine ambayo hakuyajua. Mchezo mchafu ukihusisha mfanyabiashara na watumishi wa taasisi zile za wafanyakazi wale.